1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Balozi wa Pakistan anayeshikiliwa na Wataliban azungumza

20 Aprili 2008
https://p.dw.com/p/Dl4G

Dubai:

Balozi wa Pakistan nchini Afghanistan Tariq Azizuddin ambaye alikua ametoweka tangu mwezi Februari, ametokeza katika ukanda wa video kwenye taarifa ya habari ya kituo cha televisheni cha Al- Arabiya, akisema anashikiliwa na wapiganaji wa Taliban. Alisema walikua njia kwa gari kuelekea Afghanistan Februari 11, walipotekwa nyara na wapiganaji wa Mujahedeen katika mkoa wa Khyber. Balozi huyo wa Pakistan aliongeza kwamba anashikiliwa pamoja na dereva na mlinzi wake. Bw Azizuddin akaiomba serikali yake na mabalozi wa Pakistan nchini Iran na China kufanya kila linalowezekana kuyanusuru maisha yao kwa kutekeleza madai ya Mujahedeen na Wataliban, ambayo ni pamoja na kuachiwa huru wafuasi wao waliokamatwa nchini Pakistan. Serikali ya Pakistan imesema kupigania kuachiwa huru balozi hiyo, kunapewa kipa umbele .