Bale: ″Ukame wa mabao″ haunishtui | Michezo | DW | 11.06.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Bale: "Ukame wa mabao" haunishtui

Gareth Bale kamwe hashtushwi na ukame wa mabao ya kimataifa, wakati ambapo timu ya Wales inapoingia dimbani kwa mechi ya ufunguzi dhidi ya Switzerland.

Nahodha wa timu ya Wales Gareth Bale amesema hashtushwi na ukame wake wa mabao katika mechi za kimataifa saa chache kabla ya mechi ya ufunguzi dhidi ya Uswisi. Soma zaidi Lijue kundi C la michuano ya Euro 2020

Mara ya mwisho kwa Bale kuifungia Wales ilikuwa Oktoba 2019 dhidi ya Croatia lakini amefanikiwa kuchangia katika mabao manne katika mechi saba alizojumuishwa. 

Hana wasiwasi

Fußball Stars, deren Teams sich nicht für die WM qualifiziert haben | Bale Wales

Gareth Bale

"Haijalishi. Nimefanya usaidizi. Bado ninachangia. Sina wasiwasi, kama nafasi itatokea kupata bao, nitaitumia," alisema Bale.

Siku ya Jumamosi Wales itacheza mechi ya ufunguzi dhidi ya Switzerland.

Mshambuliaji huyo wa Real Madrid, ambaye alitumia msimu uliopita kwa mkopo huko Tottenham, amefunga mabao 33 katika mechi 92 za kimataifa tangu 2006 lakini katika mechi 11 amekuwa na ukame. Bale huenda akakamilisha maisha ya soka Madrid

"Sio mwisho wa ulimwengu. Ikiwa hafungi anawasilisha mabao, muhimu asaidie kuunda mabao, anafanya hivyo." alisema kocha wa Wales, Robert Page.

AFP