1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAIDOA: Wanajeshi wa Somalia wawafukuza wanamgambo wa kiislamu

9 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4U

Wanajeshi wa Somalia wakisaidiwa na wanajeshi wa Ethiopia leo wamewalazimisha wanamgambo wa kiislamu walio na mafungamano na makahama za kiislamu waondoke kutoka mji wa Bur Hakaba, ulio karibu na makao makuu ya serikali ya mpito ya Somalia mjini Baidoa.

Mamia ya wanajeshi wa Ethiopia na wanajeshi wa serikali ya mpito waliokuwa na silaha nzito, waliingia mjini Bur Hakaba, hatua iliyowalazimu wanamgambo wakimbie.

Kwa mara ya kwanza wanamgambo wa kiislamu ambao wamekuwa wakiyateka maeneo ya kusini mwa Somalia na tayari wanaudhibiti mji mkuu Mogadishu, wameshindwa.

Waziri mkuu wa serikali ya mpito ya Somalia, Ali Mohamed Gedi, anasema wanamgambo wa kiislamu wanataka kuuvamia mji wa Baidoa.

Kenya na Ethiopia zimesema ziko tayari kusaidia kuulinda mji wa Baidoa iwapo kutakuwa na haja ya kufanya hivyo.