1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:WaIraqi hawana imani na mustakabal wao

19 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCHP

Kura mpya ya maoni iliyoafanywa nchini Iraq inaonyesha kuwa raia wa Iraq hawana imani na mustakabal wao.Miaka minne baada ya Marekani kuvamia Iraq asilimia 39 pekee ya raia wa Iraq waliohojiwa wanafurahia maisha yao.

Matokeo ya kura hiyo ya maoni yanatofautiana sana na yale yaliyofanywa na Shirika la Utangazaji la BBC mwaka 2005 yaliyoonyesha kuwa walikuwa na imani kuwa maisha yao yangebadilika.Kura hiyo ya maoni ilifanywa na shirika la habari la BBC na kituo cha Televisheni cha ABC kilichoko Marekani na kuwahusisha zaidi ya watu alfu 2.

Wakati huohuo rais wa marekani George W Bush anatarajiwa kutoa taarifa rasmi mahsusi kwa kumbukumbu ya miaka minne tangu marekani kuvamia Iraq.

Bwana Bush anayeshinikizwa na wanachama wa Democratik kuondoa majeshi yake nchini Iraq anatarajiwa kutetea mkakati wake wa kupeleka majeshi zaidi ya alfu 20 ili kudumisha amani mjini Baghdad.