1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Ujerumani yapewa siku zaidi kabla ya raia mareka wa nchi hiyo kuchinjwa

3 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCr

Wateka nyara wanaowashikilia raia wawili wa Ujerumani mama na mwanaye wameipa siku kumi zaidi Serikali ya Ujerumani kutimiza masharti yao kabla ya kuwaachia huru.

Watekaji nyara hao wamesema kuwa watawaua raia hao iwapo Ujerumani haitaondoa majeshi yake huko Afghanistan ndani ya siku kumi.

Katika mkanda wa video uliyotolewa na watekaji hao, Hanerole Krause mwenye umri wa miaka 61 ameiomba serikali ya Ujerumani kutekeleza matakwa ya watekaji hao ili kunusuru maisha yake na mwanaye.

Krause akiwa na mwanaye wa kiume mwenye umri wa miaka 20 walitekwa nyara mjini Baghdad miezi miwili iliyopita.