BAGHDAD:Saddam Hussein awatolea mwito wairaq waungane na wasameheane | Habari za Ulimwengu | DW | 08.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Saddam Hussein awatolea mwito wairaq waungane na wasameheane

Kiongozi wa zamani wa Iraq Saddam Hussein ambaye amehukumiwa kunyongwa kwa kupatikana na hatia ya uhalifu dhidi ya binadamu,amewatolea mwito wananchi wa Iraq kuungana na kusameheana kuijenga nchi hiyo.

Saddam ametoa mwito huo hapo jana alipokuwa mahakamani kusikiliza kesi ya pili inayomkabili ya mauaji ya wakurdi.

Katika kesi hiyo kiongozi huyo wa zamani pamoja na wenzake 6 wanakabiliwa na mashtaka ya mauji ya halaiki yanayohusishwa na kampeini ya mwaka 1988 dhidi ya wakurdi ambapo inasemekana zaidi ya watu 180,000 waliuwawa katika kile kinachoitwa mauaji ya Anfal.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com