BAGHDAD.Milipuko miwili ya mabomu yauwa watu 34 | Habari za Ulimwengu | DW | 30.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD.Milipuko miwili ya mabomu yauwa watu 34

Nchini Irak milipuko miwili ya mabomu imewauwa mahujaji 34 wa Kishia waliokuwa wanadhimisha sherehe za kidini za Ashura.

Mlipuko wa kwanza wa bomu lililokuwa ndani ya pipa la takataka katika mji wa Kikurdi wa Khanakin ulio kaibu na mpaka wa Iran umewauwa takriban watu 11.

Watu wengine 23 zaidi waliuwawa katika mji wa Mandali wakati mlipuaji wa kujitoa muhanga alipojilipua kwenye lango la msikiti wa Kishia mahala ambapo mahujaji wengi walikusanyika kuhudhuria kilele cha maadhimisho ya Ashura.

Takriban watu 60 wamejeruhiwa kufuatia milipuko hiyo.

Leo ni siku tukufu katika kalenda ya kiislamu na hasa kwa wafuasi wa madhehebu ya Kishia na pia ni siku ya kuadhimisha karne ya saba tangu kufariki kwa imamu Hussein mjukuu wa mtume Muhammad S.A.W.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com