BAGHDAD:Mashambulio ya mabomu yagharimu maisha ya wengi Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 09.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Mashambulio ya mabomu yagharimu maisha ya wengi Iraq

Nchini Iraq mauaji yanaendelea kushuhudiwa.Shirika la habari la Reuters limefahamisha kwamba mshambuliaji wa kujitoa muhanga amejiripua ndani ya gari na kuua wairaqi 23 waliokuwa wamejiandikisha jeshini na kujeruhi wengine 27 kusini mwa mji wa Baghdad.

Mapema watu sita waliuwawa na wengine 11 wakajehiwa kwenye mashambulio ya mabomu yakutegwa ndani ya gari kwenye eneo lililona shughuli nyingi katika wilaya ya Karrada.

Mashambulio hayo yamefuatia mengine siku ya jumamosi ambapo zaidi ya watu 150 waliuwawa na kiasi cha wengine 250 kujerihiwa baada ya bomu la kutegwa ndani ya gari kuripuliwa katika kijiji kidogo cha Tuz Khurmatu kaskazini mwa nchi watu wengine 20 hadi sasa hawajulikana waliko.Shambulio hilo ndilo baya kabisa tangu mwezi April ambapo kumeongozeka mashambulio yanayowalenga washia mjini Baghdad.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com