BAGHDAD:Mapigano yapamba moto Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 20.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Mapigano yapamba moto Iraq

Polisi ya Iraq imesema takriban watu 78 wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya bomu la kutegwa ndani ya gari kuripuka karibu na msikiti wa washia mjini Baghdad.

Shambulio hilo limetokea siku mbili tu baada ya kuondolewa kwa amri ya kutotoka nje mjini humo.

Amri hiyo ilitangazwa kufuatia shambulio dhidi ya msikiti wa dhahabu wa washia mjini Sammarra ili kuzuia ghasia za kulipiziana kisasi.

Taarifa nyingine zinasema wanajeshi wa Marekani wamewauwa watu 23 wanaoshukiwa kuwa wanamgambo.

Hii imefuatia opresheni iliyoanzishwa na wanajeshi hao dhidi ya wapiganaji wa kundi la Alqaeda na wanamgambo wakisunni katika mji wa Baquba.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com