BAGHDAD:Makombora yashambulia eneo la Iskandariya | Habari za Ulimwengu | DW | 17.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Makombora yashambulia eneo la Iskandariya

Makombora yameshambulia eneo moja mjini Baghadad hii leo na kusababisha kifo cha mwanamke mmoja na kujeruhi watu wengine 10.Eneo la Iskandariya lililo kilomita 50 kutoka mji wa Baghdad lilishambuliwa kwa makombora kulingana na duru za polisi.Kulingana na polisi hao mwili wa polisi mmoja wa Iraq ulipatikana ukininginia huku ukiwa umekatwa miguu na mikono siku mbili baada ya kutekwa kusini mwa mji mkuu.

Ghasia hizo zilianza tena siku moja baada ya raia 142 wa Iraq kupatikana wakiwa wamekufa katika kile kinachodhaniwa kuwa ghasia zilizo na misingi ya kidini kati ya Wasunni na Washia.Kwa mujibu wa polisi idadi ya watu waliokufa katika shambulio la bomu katika Chuo Kikuu cha al Mustansiriyah imeongezeka hadi 70 huku wengine zaidi ya mia moja kujeruhiwa.Hali hiyo inatokea wakati Umoja wa Mataifa imetoa tathmini ya idadi ya vifo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com