BAGHDAD:Maangamizi ya watu 200 | Habari za Ulimwengu | DW | 19.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Maangamizi ya watu 200

Watu wapatao 200 wameuawa mjini Baghdad katika mfululizo wa mashambulio yasiyokuwa na mithili tokea majeshi ya Marekani yaanze kampeni ya kuudhibiti mji huo.

Katika shambulio la bomu lililotegwa ndani ya gari watu 140 waliuawa sokoni katika mkoa wa Sadriya.

Katika shambulio jingine watu 35 waliangamia baada ya bomu kulipuka ndani ya gari kwenye kituo cha udhibiti katika mji wa Sadr.

Bomu jingine lililotegwa ndani ya gari liliua watu 11 karibu na hospitali katika mkoa wa Karada mashariki mwa mji wa Baghdad na katika mkoa mwingine wa al- Shurja watu wengine wawili waliuliwa.

Mauaji hayo yametokea wakati ambapo waziri mkuu wa Irak bwana Nuri Maliki amesema kuwa majeshi ya Irak yatakuwa tayari kuchukua jukumu la kudhibiti usalama wa nchi hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Waziri Mkuu Nuri Maliki amelaani mauaji hayo na amesema waliofanya ni askari wa shetani na ametoa agizo la kukamatwa kamanda wa mkoa wa Sadriya ambapo watu 140 waliauliwa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com