BAGHDAD:Kitisho cha Uturuki dhidi ya PKK chazidi kuzua mjadala na jazba Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 20.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Kitisho cha Uturuki dhidi ya PKK chazidi kuzua mjadala na jazba Iraq

Bunge la Iraq leo limejadili muswaada unaolaani kitisho cha Uturiki cha kutaka kufanya mashambulio dhidi ya waasi wa Kikurdi kaskazini mwa Iraq.Hata hivyo wabunge hao wameshindwa kukubaliano juu ya muswaada huo.Kamati ya rais iliyoandaa muswaada huo imetakiwa kufanya marekebisho kadhaa ili muswaada huo upigiwe kura kesho au kesho kutwa.

Kutofautiana kwa wabunge wa Iraq juu ya muswaada huo unaolaani hatua ya bunge la Uturuki ya kuidhinisha uvamizi dhidi ya waasi wa PKK kumezuka wakati baadhi ya wabunge wakisema hatua hiyo itavuruga zaidi uhusiano kati ya nchi hizo mbili.Wakati huo huo wakurdi katika eneo hilo la kaszaini mwa Iraq wameandamana kupinga kitisho cha Uturuki wakionya kwamba watakuwa tayari kutetea jimbo lao.Kwa upande mwingine waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kwamba mwenzake Nuri al Maliki amependekeza hatua ya pamoja kuwakabili waasi wa kikurdi wa PKK.Erdogan pia ameilaumu Marekani kwa kuwa chanzo cha kukita kwa kambi ya waasi hao nchini Iraq na amesema mazungumzo yake na rais Bush mwezi ujao yatakuwa muhimu katika kuamua hatua itakayochukuliwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com