BAGHDAD:Kifo cha Saddam chazusha hisia mbali mbali | Habari za Ulimwengu | DW | 31.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Kifo cha Saddam chazusha hisia mbali mbali

Kumekuwepo na hisia Tofauti juu ya kunyongwa kwa Saddam Hussein.

Rais wa Marekani Gorge W Bush ameieleza hatua hiyo kama hatua muhimu kwa Iraq .

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Margaret Beckett amesema kiongozi huyo wa zamani wa Iraq amewajibika kwa baadhi ya uhalifu alioutekeleza dhidi ya watu wa Iraq.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amefahamisha kwamba serikali yake inapinga kabisa hukumu ya kifo na kwa hivyo haijafurahishwa na kitendo hicho dhidi ya rais wa zamani wa Iraq lakini wakati huo huo Ujerumani imesema Saddam alikutwa na hatia ya uhalifu wa kivita wairaq wanapasa kuweka amani na kushikamana kuijenga nchi yao.

Urussi halikadhalika imekosoa tukio hilo lakini imewataka wairaq waweke amani na utulivu.Mashirika ya kutetea haki za binadamu yametoa sauti zao,shirika la Amnesty International limesema kesi dhidi ya Saddam ilijawa na dosari na kuingiliwa kisiasa.

Katika mashariki ya kati nchini Palestina vyama vya Hamas na Fatah vimelaani kitendo hicho na kukitaja kuwa mauaji ya kisiasa.Saudi Arabia imekosowa juu ya hukumu hiyo kutekelezwa siku ya kwanza ya sikukuu kubwa ya kiislamu ya Eid al Adha.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com