1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Kampuni ya usalama ya Marekani yafungiwa leseni

17 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOy

Wizara ya mambo ya ndani ya Irak imesimamisha mara moja leseni ya kampuni ya usalama ya Marekani ya Blackwater baada ya msafara wa kidiplomasia wa Marekani kushambuliwa kwa risasi siku ya jumapili.

Takriban watu wanane waliokuwa kando ya barabara waliuwawa kwenye shambulio hilo wakati mawakala wa usalama walipojibu mashambulio ya risasi katika eneo la Al Nissur magharibi mwa mji wa Baghdad.

Watu kumi na tatu walijeruhiwa kwenye shambulio hilo.

Taarifa kutoka wizara ya mambo ya ndani mjini Baghdad imesema kwamba uchunguzi zaidi unafanywa kuhusiana na tukio hilo.