1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD.Idadi ya vifo vya raia imeongezeka nchini Irak

22 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCqN

Idadi ya vifo vya raia nchini Irak imeongezeka na kufikia watu 3,709 hadi kufikia mwezi wa oktoba mwaka huu wa 2006.

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na umoja wa mataifa ambayo inasema kuwa vifo hivyo vimesababishwa zaidi na mauaji yanayoendelea kati ya Wasunni na Washia nchini Irak.

Mauaji hayo yamesababisha umasikini mkubwa miongoni mwa jamii hizo.

Zaidi ya raia laki nne wa Irak hawana makaazi ya kudumu tangu shambulio la bomu la mwezi februari dhidi ya mahala patakatifu pa jamii ya Washia katika mji wa Samara.

Takriban Wairak laki moja wanakimbilia nchini Syria na Jordan kila mwezi.

Raia wa Irak milioni 1.6 wameshakimbia kutoka nchini mwao tangu majeshi ya Marekani yalipoiovamia Irak mwaka 2003.