1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:helikopta nyingineya Marekani yaanguka nchini Irak,saba wafa

8 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCU9

Helikopta ya jeshi la Marekani aina ya Sea Knight imeunguka karibu na mji wa Baghdad na watu wote saba waliokuwamo ndani yake wamekufa.

Jeshi la Marekani limesema kuwa sababu ya kuanguka helikopta hiyo bado inachunguzwa.

Lakini afisa wa jeshi la anga la Irak amesema kuwa helikopta hiyo iliangushwa kwa kombora.

Hiyo ni helikopta ya tano ya jeshi la Marekani kuanguka mnamo muda wa wiki nne nchini Irak.