BAGHDAD:Dawa yazidi kumwagika nchini Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 03.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Dawa yazidi kumwagika nchini Iraq

Watu 15 wameuawa akiwemo askari mmoja wa Marekani na wengine zaidi ya mia mbili kujeruhiwa baada ya mtu wa kujitoa mhanga kujilipua akiwa ndani ya gari katika mji wa Kirkuk nchini Iraq

Mtu huyo alilibamiza gari lililokuwa na mabomu kwenye kituo cha Polisi, ambapo mbali ya askari huyo wa Marekani, pia askari wawili wa Iraq waliuawa.

Polisi pia wamesema kuwa wameokota maiti 21 hapo jana katika mji wa Baqouba ambao uko nje kidogo ya Baghdad.

Mjini Baghdad kwenyewe, mapema leo watu watatu wameuawa baada ya bomu lililotegwa pembezoni mwa barabara kulipuka.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com