BAGHDAD: Watu zaidi ya 40 wauwawa kwenye mashambulio | Habari za Ulimwengu | DW | 01.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Watu zaidi ya 40 wauwawa kwenye mashambulio

Polisi nchini Irak wamesema watu waliokuwa wamejihami na bunduki wamelishambulia basi la abiria mapema leo katika kitongoji cha Iskandariya, kusini mwa mji mkuu Baghdad na kuwaua watu 11 akiwemo mwanamke mmoja na mtoto.

Kaskazini mwa Baghdad, mtu wa kujitoa mhanga maisha amewaua watu zaidi ya 32 kwenye matanga ya Washia.

Polisi wa Irak wanasema shambulio hilo lilifanywa ndani ya hema lililokuwa na watu wengi katika mji wa Khalis kwenye wilaya ya Diayala. Watu zaidi ya 60 walijeruhiwa kwenye hujuma hiyo.

Sambamba na taarifa hizo, jeshi la Marekani nchini Irak linasema wanajeshi wake wanne waliuwawa mjini Baghdad mwishoni mwa juma lililopita hivyo kuiongeza idadi ya wanajeshi wake waliouwawa mwezi Aprili kufikia zaidi ya 100.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com