BAGHDAD: Watu saba wakiwemo wanajeshi watatu wauwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 31.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Watu saba wakiwemo wanajeshi watatu wauwawa

Wapiganaji nchini Irak leo wamewaua watu wasiopungua saba wakiwemo wanajeshi watatu wa Irak. Duru zinasema genge la watu waliokuwa na bunduki walikivamia kituo cha upekuzi cha jeshi la Irak mjini Hawijah, magharibi mwa Kirkuk.

Kamanda wa polisi wa eneo hilo, Atallah Mahmud, amesema wanajeshi watatu wameuwawa na wengine wawili wakajeruhiwa vibaya katika hujuma hiyo.

Wairaki wawili waliuwawa na wengine wawili wakajeruhiwa wakati wanamgambo walipovurumisha roketi aina ya Kyatusha kwenye wilaya ya Washia ya Kadhimiyah kaskazini mwa Baghdad, ambako rais wa zamani wa Irak, Saddam Hussein alitiwa kitanzi.

Muiraki mwingine ameuwawa na wengine sita wakajeruhiwa kwenye mripuko wa bomu lililokuwa limetegwa ndani ya motokaa katika kitongoji cha Hurriyah mjini Baghdad.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com