BAGHDAD: Watu 10 wameuwawa katika mashambulio ya mabomu | Habari za Ulimwengu | DW | 23.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Watu 10 wameuwawa katika mashambulio ya mabomu

Takriban watu 10 wameuwawa kufuatia mashambulio mawili ya mabomu kwa wakati mmoja yaliyofanyika katikati ya mji mkuu wa Baghdad nchini Irak.

Watu wengine 15 wamejeruhiwa katika mashambulio hayo.

Washambuliaji wa kujitoa muhanga walilipua bomu lakwanza karibu na ofisi ya serikali katika kitongoji cha Karrada ambapo vitambulisho vinatolewa.

Bomu jingine lililipuka kwenye sehemu ya maduka inayokaliwa na jamii ya washia.

Eneo la Karrada limekuwa likikumbwa na mashambulio ya mara kwa mara katika siku za hivi karibuni.

Jeshi la Marekani pia limetowa taarifa juu ya kuuwawa kwa mwanajeshi wake mmoja kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya shambulio la bomu la kutegwa kando ya barabara siku ya jumapili.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com