BAGHDAD: Wanamgambo wa Kishia wamekamtwa Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 19.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Wanamgambo wa Kishia wamekamtwa Irak

Mashambulio mapya ya bomu nchini Irak yameua hadi watu 20.Katika mji mkuu Baghdad,mabomu matatu ya gari yaliripuka katika muda wa dakika chache,karibu na soko lililo katika mtaa wa Dora ambako Wasunni wengi huishi.Kwa mujibu wa polisi si chini ya watu 10 waliuawa katika miripuko hiyo na wengine 30 walijeruhiwa.Kwa upande mwingine waziri mkuu wa Irak,Nouri al-Maliki amesema,zaidi ya wanamgambo 400 wa Kishia wa Jeshi la Mahdi walikamtwa katika kipindi cha majuma machache ya nyuma.Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa serikali kueleza juu ya hatua zilizochukuliwa na vikosi vya usalama dhidi ya wanamgambo wa shehe wa Kishia mwenye msimamo mkali-Moqtada al-Sadr.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com