BAGHDAD: Wanajeshi sita wa Marekani wauwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 02.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Wanajeshi sita wa Marekani wauwawa

Wanajeshi sita wa Marekani wameuwawa katika shambulio la bomu la kutegwa kando ya barabara kusini magharibi mwa mji wa Baghdad.

Mashambulio hayo yanatoa wakati mgumu kwa vikosi vya Irak na Marekani tangu vilipoanzisha operesheni dhidi ya wapiganaji wenye msimamo mkali katika mji wa Baghdad kati kati ya mwezi Februari.

Watu wawili wameuwawa katika mashambulio ya mabomu ya kutegwa ndani ya magari. Mashambulio hayo pia yamewajeruhi watu 17 katika kambi ya kijeshi ya kaskazini mwa mji wa Mosul kwa mujibu wa taarifa ya polisi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com