BAGHDAD: Wanajeshi 4 wa Marekani wauawa Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 19.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Wanajeshi 4 wa Marekani wauawa Irak

Wanajeshi 4 wa Kimarekani na mkalimani wao wameuawa katika shambulizi la bomu nchini Irak. Bomu hilo lilitegwa na waasi kando ya barabara, mashariki ya mji mkuu Baghdad.Sasa idadi ya wanajeshi wa Kimarekani waliopoteza maisha yao nchini Irak katika mwezi huu peke yake,imefikia 47.Wakati huo huo chama cha Republikan katika Seneti ya Marekani kimezuia jeribio jingine la Wademokrat kumlazimisha Rais George W.Bush akubali kuvirejesha vikosi nyumbani hadi ifikapo April mwakani.Pendekezo la chama cha Demokrat liliungwa mkono kwa kura 52 na 47 zilipinga,kwa hivyo halikupata uwingi wa kura 60 zinazohitajiwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com