BAGHDAD: Umwagaji wa damu waendelea Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 27.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Umwagaji wa damu waendelea Irak

Watu wasiopungua 12 wameuawa,baada ya bomu lililotegwa ndani ya gari,kuripuka karibu na soko mjini Baghdad.Shambulizi hilo katika mtaa wanakoishi Washia wengi,limejeruhi zaidi ya watu 60.Mashambulizi mengine ya mabomu yaliyotegwa ndani ya gari,katika miji ya Kirkuk na Hilla yameua jumla ya watu 11,ikiwa ni pamoja na askaripolisi 5 wa Kiiraqi.

Wakati huo huo,idadi ya mashabiki wa kandanda wa Kiiraqi waliouawa katika mashambulizi mawili ya mabomu yaliyotegwa ndani ya gari,imefikia 50.Mashambulizi hayo yamejeruhi pia watu wapatao 90.Washabiki hao wa mpira,walikuwa wakisherehekea ushindi wa timu ya Iraq dhidi ya Korea ya Kusini, katika nusu fainali ya Kombe la Asia siku ya Jumatano.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com