BAGHDAD : Uchunguzi wa mripuko wa bunge wafanyika | Habari za Ulimwengu | DW | 13.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD : Uchunguzi wa mripuko wa bunge wafanyika

Uchunguzi juu ya mripuko uliotokea kwenye bunge la Iraq unaendelea kufanyika na hadi hivi sasa wafanyakazi watatu wa mkahawa wa bunge hilo lenye ulinzi mkali wamekamatwa.

Hassan al Senaid kutoka muungano wa kundi tawala la Mashia amesema baadhi ya walinzi wa bunge pia wamekuwa wakichuchunguzwa lakini hakuna anaeshikiliwa.

Bunge limekuwa na kikao maalum leo hii kulaani kuripuliwa kwa bunge hilo hapo jana ambapo jeshi la Marekani linasema watu wanane wameuwawa wakati mshambuliaji wa kujitolea muhanga maisha alipojipenyeza na kukwepa vituo kadhaa vya ukaguzi na kujiripuwa mkahawani wakati wabumge wakijipatia chakula chao cha mchana.

Wabunge watatu ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha yao katika mripuko huo ambao umewajeruhi zaidi ya watu 20.

Mripuko huo katika bunge hilo Iraq unakuja siku moja baada ya waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates kuelezea uwezekano wa kupunguza wanajeshi wa Marekani walioko nchini Iraq kufikia mwishoni mwa mwaka 2007 au mapema mwaka 2008.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com