1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Uamuzi wa Moqtada al-Sadr wakaribishwa

1 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTh

Vikosi vya Marekani na Irak hii leo vimevamia ngome ya Moqtada al-Sadr katika mji wa Baghdad. Watu 3 walikamatwa katika msako wa nyumba mbili kwenye mtaa wa Sadr City ambako kuna umasikini wanaishi kiasi ya Washia milioni moja,wengi wao wakiwa wafuasi wa al-Sadr.

Uvamizi huo ulifanywa saa chache kabla ya wakuu wa majeshi ya Marekani kutoa taarifa ya kukaribisha uamuzi wa kiongozi wa madhehebu ya Kishia,Moqtada al-Sadr,kusitisha harakati za wanamgambo wake wa Jeshi la Mahdi.

Siku ya Jumatano Moqtada al-Sadr alitoa amri kwa wanamgambo wa Jeshi la Mahdi,kusitisha harakati zake zote,ikiwa ni pamoja na mashambulizi dhidi ya vikosi vinavyoongozwa na Marekani.