1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Talabani amepinga mapendekezo katika ripoti ya Marekani

11 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCkS

Rais wa Irak,Jalal Talabani ameyapinga mapendekezo ya jopo la wanasiasa mashuhuri wa Kimarekani,kuhusu mabadiliko ya kufanywa katika sera ya Marekani nchini Irak.Talabani aliwaambia waandishi wa habari kuwa ripoti hiyo sio ya haki na itadhoofisha mamlaka ya Irak.Miongoni mwa mapendekezo yaliyotolewa ni kufungamanisha msaada wa nchi za magharibi na maendeleo yanayofanywa na serikali kuhusu usalama na vile vile kuwahusisha wanachama wa chama cha Baath cha rais wa zamani Saddam Hussein katika utaratibu wa upatanisho. Ripoti zingine zinasema,watu wenye silaha walivamia nyumba mbili mjini Baghdad na wakawaua watu tisa wa familia mbili za Kishia katika mtaa wanakoishi Wasunni wengi zaidi.