BAGHDAD: Shambulio limeua watu 33 nchini Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 07.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Shambulio limeua watu 33 nchini Iraq

Si chini ya watu 33 wameuawa nchini Iraq,baada ya bomu lililotegwa kwenye gari kuripuka karibu ya soko lililojaa watu kwenye eneo la Baghdad ambako Washia wengi huishi.Katika siku za hivi karibuni, eneo la Bayya,mara kwa mara limeshuhudia mashambulio ya kimadhehebu.Kwa upande mwingine vikosi vya Marekani vimewaua wanamgambo 10 katika eneo la Sadr City na kuteketeza chumba cha mateso,katika operesheni inayoendelea,katika juhudi ya kuleta usalama kwenye mji mkuu Baghdad. Na katika eneo la Samarra kaskazini mwa Baghdad,katika shambulio la kujitolea muhanga kwenye gari,wanamgambo wawili walishambulia vituo vya polisi na kuua hadi maafisa 12 ikiwa ni pamoja na kamanda wa polisi wa eneo hilo.Watu wengi pia walijeruhiwa katika shambulio hilo. Wakati huo huo,maafisa wa kijeshi wa Marekani wamesema,wanajeshi wake 8 waliuawa nchini Iraq siku ya Jumapili.Sita kati yao waliuawa katika shambulio moja lililotokea kwenye wilaya ya Diyala.Mwandishi wa habari wa kiraia pia aliuawa katika shambulio hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com