1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Sadr awaondoa mawaziri wake katika serikali.

17 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9L

Kiongozi wa kidini wa Kishia Moqtada al-Sadr ameamuru mawaziri wake kuondoka katika serikali ya muungano ya Iraq.

Kundi la Sadr ambalo lina mawaziri sita , linajaribu kumpa mbinyo waziri mkuu Nouri al Maliki kuweka muda maalum kwa majeshi ya Marekani kuondoka nchini humo.

Maliki amekataa, akisema kuwa kuondoka kwa majeshi ya Marekani kutategemea hali itakayokuwa nchini Iraq.

Sadr amekuwa akipinga kuwepo kwa majeshi ya Marekani nchini humo tangu kuangushwa kwa kiongozi wa zamani Saddam Hussein miaka minne iliyopita.

Wakati huo huo watu wenye silaha wamewauwa wanajeshi 13 wa Iraq katika kituo cha upekuzi karibu na mji wa kaskazini wa Mosul. Mwishoni mwa juma kiasi cha raia 80 waliuwawa na wapiganaji kwa mabomu nchini humo.