Baghdad. Saddam aawaaga Wairaq. | Habari za Ulimwengu | DW | 28.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Baghdad. Saddam aawaaga Wairaq.

Rais wa zamani wa Iraq Saddam Hussein amewataka Wairaq kuungana na kupambana na majeshi ya Marekani nchini humo. Katika barua ya kuaga iliyoandikwa kutoka katika chumba amofungiwa , Saddam pia amesema kuuwawa kwake kutamfanya kuwa shahidi mkuu. Upande wa utetezi katika kesi ya Saddam umesema kuwa ameelekeza kuandikwa kwa barua hiyo mwezi uliopita, muda mfupi baada ya kutolewa hukumu ya kifo dhidi yake kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Mapema wiki hii, mahakama ya rufaa ilikubali hukumu hiyo ya kifo na kuamua kuwa Saddam anyongwe katika muda wa siku 30.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com