BAGHDAD : Rumsfeld azuru wanajeshi Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 10.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD : Rumsfeld azuru wanajeshi Iraq

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld ambaye yuko njiani kun’gatuka amefanya ziara ya ghafla nchini Iraq kuwashukuru wanajeshi wa Marekani kwa huduma zao kwa taifa.

Akizungumza na wanamaji walioko kwenye jimbo tete la Anbar Rumsfeld amesema imekuwa ni bahati kwake kufanya kazi na wanajeshi hao wake kwa waume.Safari yake imekuja siku mbili baada ya jopo la vigogo wa Marekani kuonya kwamba mwelekeo mpya unahitajika kwa Iraq kuzuwiya hali ilio mbaya nchini humo kuzidi kuwa mbaya zaidi.Rumsfeld amejiuzulu hapo mwezi wa Novemba siku moja baada ya chama cha Rais George W.Bush cha Republican kupoteza udhibiti wa bunge la Marekani katika uchaguzi mada kuu ikiwa ni vita vya Iraq.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com