BAGHDAD: Raia zaidi waliuwawa katika shambulio la risasi | Habari za Ulimwengu | DW | 08.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Raia zaidi waliuwawa katika shambulio la risasi

Viongozi wawili wa Kishia wametiliana saini mapatano ya kuzuia mauaji.

Viongozi hao Moqtada al Sadr na Abdulaziz al Hakim wamekuwa wanapambana vikali katika kuwania udhibiti wa sehemu zinazokaliwa hasa na Washia.

Mapambano baina ya jamii tofauti nchini Irak yanakwamisha juhudi za waziri mkuu Nouri al Maliki zenye lengo la kuleta mageuzi yanayotakiwa na Marekani.

Wakati huo huo serikali ya Irak imetoa taarifa kwamba watu zaidi waliuwawa katika shambulio la risasi la mwezi uliopita lililotekelezwa na mawakala wa usalama wa kampuni ya kimarekani ya Black Water katika mji wa Baghdad.

Awali ilisemekana kuwa ni watu 11 waliouwawa lakini wachunguzi wa Irak wamesema ni watu 17 waliouwawa ilihali maafisa wa kampuni hiyo hawakuchukuliwa hatua zozote.

Aidha matokeo ya uchunguzi huo yameonyesha kuwa maafisa hao wa kampuni ya usalama ya Black Water waliwauwa raia wa Irak kimakusudi na wala hawakukabiliwa na vitisho vya aaina yoyote.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com