BAGHDAD: Nuri al Maliki azuru Ramadi | Habari za Ulimwengu | DW | 13.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Nuri al Maliki azuru Ramadi

Waziri mkuu wa Irak, Nuri al Maliki ameutembelea mji wa Ramadi magharibi mwa Irak katika ziara ambayo haikutangazwa.

Ziara hiyo ni ya kwanza ya kiongozi huyo wa kishia kuzuru ngome ya wapiganaji wa kisuhhi, yapata kilomita 110 magharibi mwa mji mkuu Baghdad.

Nuri al Maliki amekutana na viongozi wa eneo hilo, maafisa wa serikali na makamanda wa Irak pamoja na vikosi vya usalama mjini humo.

Ziara ya waziri mkuu huyo inafanyika wakati vikosi vya Marekani na vya Irak vikiendelea na kampeni ya kuzima machafuko mjini Baghdad.

Wakati haya yakiarifiwa rais wa Irak, Jalal Talabani ambaye amekuwa akiendelea kupata matibabu katika hospitali moja mjini Amman nchini Jordan, anatarajiwa kuondoka hospitalini hapo kesho na kurejea nchini Irak.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com