Baghdad. Nouri al-Maliki awashutumu Wasunni . | Habari za Ulimwengu | DW | 13.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Baghdad. Nouri al-Maliki awashutumu Wasunni .

Waziri mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki amewalaumu wasunni wenye msimamo mkali na wale wanaomuunga mkono dikteta wa zamani Saddam Hussein kwa shambulio baya kabisa la bomu dhidi ya soko moja mjini Baghdad jana asubuhi.

Zaidi ya watu 70 , wengi wao wakiwa masikini kutoka katika jamii ya Washia wameuwawa wakati mshambuliaji wa kujitoa muhanga alipolipua gari lake katika kundi la wafanyakazi vibarua wanaotafuta ajira katika mji huo.

Zaidi ya watu 200 wamejeruhiwa.

Iraq imekumbwa na machafuko ya kimadhehebu baina ya Washia na Wasunni kwa muda mwingi wa mwaka huu. Kutokana na machafuko hayo, rais wa Marekani George W. Bush anatarajiwa kupitia upya sera za utawala wake nchini Iraq mapema mwaka ujao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com