1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Moqtada Sadr asitisha harakati za jeshi lake

30 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBUP

Sheikh wa msimamo mkali wa madhehebu ya Shia nchini Iraq Moqtada al Sadr ametangaza kwamba wanamgmabo wa jeshi lake la Mahdi watasitisha harakati zao zote kwa kipindi cha miezi sita.

Sadr ametowa agizo hilo kufuatia mapigano ya siku mbili kwenye mji mtakatifu wa Washia wa Karbala ambapo watu zaidi ya 50 wameuwawa na maelfu ya mahujaji kuukimbia mji huo. Mapigano hayo yalikuwa kati ya wapiganaji walio tiifu kwa Sadr na polisi wenye mafungamano na kundi hasimu la kisiasa la Mashia linalojulikana kama Baraza Kuu la Kiislam nchini Iraq.

Waziri Mkuu wa Iraq Nuri al Maliki ametengaza amri ya kutotembea nje kwenye mji huo na amepelekea wanajeshi kuimarisha usalama.