1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD :Mlipuko sokoni waua 18 helikopta zadondoka

15 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9j

Mabomu mawili ya kutegwa garini yamelipuka katika soko moja mjini Baghdad na kusababisha vifo vya yapata watu 18 na kujeruhi wengine 50.Mabomu hayo yalilipuka moja baada ya jingine katika kipindi cha dakika tano kwenye eneo lililo na Washia wengi.Wakati huohuo helikopta mbili za Marekani zilidondoka baada ya kugongana hewani na kusababisha vifo vya wanajeshi wawili na wengine watano kujeruhiwa kwa mujibu wa duru za kijeshi.

Mlipuko huo wa sokoni ulianzisha tena vifo vilivyo na misingi ya kidini ikiwa ni siku moja baada ya bomu moja kusababisha vifo vya watu takriban 37 na kujeruhi wengine 150 karibu na kituo cha basi.Eneo hilo liko karibu na msikiti la Karbala.

Mbali na vifo hivyo,takriban watu wengine 40 waliuawa au kupatikana wakiwa wamekufa nchini Iraq hapo jana.Kundi moja linalohusika na kundi la kigaidi la Al Qaeda lilitoa taarifa katika mtandao inayodai kuwa waliwateka wanajeshi 20 wa Iraq ili kulipiza kisasi kifo cha mwanamke mmoja kilichosababishwa na polisi.