BAGHDAD :Mlipuko darajani waua 10 | Habari za Ulimwengu | DW | 12.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD :Mlipuko darajani waua 10

Lori moja limeripuka kwenye daraja moja kuu mjini Baghdad mapema hii leo na kusababisha magari kadhaa kuzama katika mto Tigris.Kwa mujibu wa polisi yapata watu 10 waliuawa na wengine 26 kujeruhiwa na kulingana na maafisa wa hospitali idadi hiyo huenda ikaongezeka.Polisi wanaendelea na juhudi za kuokoa manusura baada ya magari ya watu kama 20 kuzama pale daraja lilipoanguka.

Shambulio hilo lililenga kulipua daraja la al-Sarafiya linalounganisha mitaa ya Waziriyah na Utafiyah ya Baghdad ambayo ni maeneo ya Sunni na Shia.Kulingana na polisi shambulio hilo lilitekelezwa na mlipuaji wa kujitolea muhanga japo picha za televisheni ya kituo cha AP zinaonyesha kuwa daraja hilo lilipasuka mara mbili jambo linaloashiria milipuko miwili.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com