BAGHDAD: Misikiti ya Kisunni yateketezwa moto. | Habari za Ulimwengu | DW | 14.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Misikiti ya Kisunni yateketezwa moto.

Misikiti mitatu ya madhehebu ya Sunni imeteketezwa moto katika mji wa Iskandariya kusini mwa Baghdad, karibu na mahali ambapo wanamgambo jana waliushambulia kwa bomu msikiti wa madhehebu ya Shia katika mji wa Samarra.

Msikiti huo wa Samarra ulishambuliwa mwezi Februari mwaka uliopita, tukio lililosababisha mapambano ya kimadhehebu.

Maelfu ya watu waliuawa kutokana na ghasia hizo za kimadhehebu.

Wanajeshi wa Iraq wakishirikiana na vikosi vya Marekani walishika doria katika barabara za Baghdad na miji mingine kuhakikisha amri iliyoweka ya kutotoka nje inafuata.

Misikiti hiyo ya kusini mwa Baghdad imeshambuliwa siku moja baada ya wakuu wa majeshi ya Marekani kutangaza wataagiza vikosi vyote vyao vishiriki kwenye misako ya kiusalama mjini Baghdad.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com