BAGHDAD : Miripuko yauwa watu zaidi ya 60 | Habari za Ulimwengu | DW | 15.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD : Miripuko yauwa watu zaidi ya 60

Miripuko kadhaa ya mabomu nchini Iraq hapo jana imeuwa zaidi ya watu 60.

Katika shambulio baya kabisa mshambuliaji wa kujitolea muhanga maisha amejiripuwa na gari kwenye kituo cha basi katika mji mtakatifu wa Washia wa Karbala na kuuwa takriban watu 43 na kujeruhi wengine zaidi ya 100.Mripuko huo umetokea karibu na eneo takatifu la Imam Hussein ambalo ni mojawapo ya maeneo matakatifu kabisa kwa Waislamu wa madhehebu ya Shia ambapo mjukuu huyo wa Mtume Muhammad SAW wa Waislamu amezikwa.

Shambulio jengine la kujitolea muhanga maisha mjini Baghdad limeuwa watu 10 wakati mashambulizi mengine ya ziada nchini kote yameuwa watu 13 na kufanya idadi ya watu waliouwawa hapo jana kufikia 66.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com