1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Mashambulio nchini Irak yameuawa hadi watu 58

12 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCK4

Si chini ya watu 58 wameuawa katika mashambulio yaliyoafanywa sehemu mbali mbali nchini Irak. Katika shambulio moja peke yake,zaidi ya watu 30 waliuawa.Kwa mujibu wa polisi,mshambulizi katika gari lenye bomu alishambulia lori lililokuwa na mahujaji wa Kishia.Katika shambulio jingine kaskazini-mashariki ya Baghdad,mshambuliaji alijiripua ndani ya basi na kuwaua watu 10 na kuwajeruhi wengi wengine.Mashambulio hayo yametokea siku moja baada ya madola makuu,Irak na nchi za jirani Iran na Syria,kukutana mjini Baghdad kutafuta njia za kuleta utulivu nchini Irak.Serikali za Syria na Iran zimesema,zipo tayari kusaidia kuleta amani katika nchi ya jirani.Marekani mara kwa mara,imezilaumu nchi hizo mbili kuwa zinatoa misaada ya kijeshi na fedha kwa waasi nchini Irak.Wajumbe kwenye mkutano huo wamekubaliana kuwa na majadiliano zaidi kwa lengo la kukomesha mapigano ya kimadhehebu.