BAGHDAD :Mashambulio Fallujah | Habari za Ulimwengu | DW | 21.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD :Mashambulio Fallujah

Majeshi ya Iraq yakishirikiana na ya Marekani yameshambulia wanamgambo wanaodhaniwa kuhusiana na Al Qaida katika mji wa Fallujah na kusababisha vifo vya wanamgambo 8 na kujeruhi polisi 5 wa Iraq.Mapigano hayo yalianza jana asubuhi pale polisi katika eneo la Amriya lililo kilomita 40 magharibi mwa Baghad waliposhambulia kambi za kijeshi kwa makombora.

Kulingana na msemaji wa kikosi hicho Luteni Kanali Roger Hollenbeck wapiganaji wawili wa Al Qaeda waliuliwa na polisi na kujeruhi wengine watano.

Polisi wa Iraq kwa upande wao waliwakamata wanamgambo 45 vilevile kupata silaha kadhaa katika msako wa nyumba hadi nyumba mjini Ramadi mkoani Anbar.Bomu moja la kutegwa ardhini lililipuka na kusababisha kifo cha raia mmoja na kuwajeruhi wengi watano.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com