BAGHDAD: Marekani yapoteza wanajeshi 8 Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 19.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Marekani yapoteza wanajeshi 8 Iraq

Wanajeshi 8 wa Kimarekani wameuawa nchini Iraq. Kwa mujibu wa maafisa wa vikosi vya Marekani,7 waliuawa katika kipindi cha siku moja huku machafuko yakipamba moto nchini humo.Wakati huo huo operesheni ya kuwasaka wanajeshi 3 Kimarekani waliotekwa nyara inaendelea kwa kasi.Sasa idadi ya wanajeshi wa Kimarekani waliouawa nchini Iraq tangu nchi hiyo kuvamiwa March mwaka 2003, imefikia 3,412.Katika mwezi huu wa Mei peke yake, Marekani imepoteza wanajeshi 69.Kwa upande mwingine,Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair anaeondoka madarakani mwisho wa mwezi Juni, amefanya ziara ya ghafula nchini Iraq.Ziara hiyo lakini imekabiliwa na habari za mauaji ya wanavijiji 16 wa Kikurd.Hata hivyo,alipozungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari baada ya kujadiliana na Waziri Mkuu wa Iraq,Nouri al-Maliki na Rais Jalal Talabani,Blair alishikilia kuwa kuna ishara za kupatikana maendeleo ya kisiasa nchini Iraq tangu Saddam Hussein kuondoshwa madarakani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com