BAGHDAD : Majeshi ya muungano yauwa waasi 10 | Habari za Ulimwengu | DW | 25.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD : Majeshi ya muungano yauwa waasi 10

Katika mashambulizi matatu ya wakati mmoja kaskazini mwa Baghdad vikosi vya muungano vimewauwa waasi 10.

Jeshi la Marekani limesema mashambulizi hayo yamekuja baada ya kugunduliwa kwa kiwanda cha kutengeneza mabomu na maficho ya silaha.Katika mapigano huko Taji kilomita 20 kaskazini mwa mji mkuu mvulana mdogo ameuwawa na mwanamke mja mzito amejeruhiwa.Mashambulizi hayo yanakuja wakati umwagaji damu wa kimadhehebu ukiendelea kupamba moto nchini kote Iraq.

Katika kile kinachoonekana dhahir kuwa ni mashambulizi ya kulipiza kisasi hapo jana takriban misikiti minne ya Wasunni na nyumba kadhaa zimetiwa mkoto na kuuwa takriban watu 25.

Wanamgambo pia waliwateka Wasunni sita wakati wakiondoka msikitini baada ya sala ya Ijumaa na kuwateketeza kwa kuwawasha na mafuta wakati wakiwa hai.

Hapo Alhamisi miripuko kadhaa ya mabomu imeuwa zaidi ya watu 215 katika wilaya ya Baghdad ya Washia ya Mji wa Sadr.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com