BAGHDAD: Majeshi ya Marekani yavamia ubalozi mdogo wa Iran katika eneo la kaskazini mwa Iraq. | Habari za Ulimwengu | DW | 11.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Majeshi ya Marekani yavamia ubalozi mdogo wa Iran katika eneo la kaskazini mwa Iraq.

Majeshi ya Marekani yamevamia ubalozi mdogo wa Iran na kuwatia nguvuni watu watano katika mji wa Wakurdi wa Arbil kaskazini mwa nchi hiyo.

Majeshi hayo pia yamechukua nyaraka na mitambo huku maafisa wa jimbo hilo wakifunga barabara zote zinazoelekea katika jengo hilo.

Mjini Tehran, serikali ya Iran imeitisha mkutano na maafisa wanaowakilisha maslahi ya Marekani nchini humo.

Majeshi ya Marekani yamechukua hatua hiyo wakati Marekani ingali ikiinyooshea kidole Iran kwamba inachochea mzozo na inawaongoza wanamgambo wanaoshambulia vikosi vyake nchini Iraq.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com