BAGHDAD: Kiongozi wa tawi la Al-Qaeda huenda ikawa amejeruhiwa | Habari za Ulimwengu | DW | 16.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Kiongozi wa tawi la Al-Qaeda huenda ikawa amejeruhiwa

Wizara ya mambo ya ndani ya Irak imenukuliwa ikisema kuwa kiongozi wa tawi la Al-Qaeda nchini Irak,Abu Ayyub al-Masri,amejeruhiwa katika mapigano na vikosi vya Kiiraki.Inasemekana kuwa mshauri wake mmoja aliuawa katika mapigano hayo, kaskazini mwa mji mkuu Baghdad.Al-Masri alie mzaliwa wa Misri,alishika uongozi wa tawi hilo la Al-Qaeda,baada ya mwanamgambo wa Kijordan Abu-Musab al-Zarqawi kuuawa Juni mwaka jana,katika shambulio la angani la Marekani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com