BAGHDAD: Kiongozi wa Al Qaeda katika jimbo la Salahuddin auwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 06.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Kiongozi wa Al Qaeda katika jimbo la Salahuddin auwawa

Jeshi la Marekani limesema kwamba limemuuwa kiongozi wa mashambulio dhidi ya madhabahu ya Kishia ya mwaka jana yaliyosababisha kuongezeka mashambulio baina ya madhehebu tafauti nchini Irak.

Jeshi la Marekani limesema Haitham al Badri alikuwa kiongozi wa kundi la Al Qaeda katika jimbo la Salahuddin.

Viongozi wa Marekani na wa Irak wanamlaumu Badri kwa kuhusika na mashambulio mawili dhidi ya msikiti wa Al Askari katika mji wa Samarra la kwanza lilifanyika mwaka 2006 na la pili lilifanyika takriban wiki saba zilizo pita.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com