BAGHDAD :Jeshi la Mahdi kusitisha shughuli zake kwa miezi sita | Habari za Ulimwengu | DW | 29.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD :Jeshi la Mahdi kusitisha shughuli zake kwa miezi sita

Kiongozi wa kidini wa Kishia aliye na msimamo mkali Moqtada al Sadr amewaamrisha wapiganaji wa jeshi lake la Mahdi kusitisha shughuli zao ili kupanga upya kikosi hicho.Kulingana

Mshauri wake mmoja Sheikh Hazim al Araji lengo la hatua hiyo kuchukuliwa ni kukarabati kundi hilo ambalo linaripotiwa kusambaratika.Marekani kwa upande wake inashikilia kuwa jeshi hilo la Mahdi linapewa mafunzo na vifaa na nchi ya Iran.

Agizo hilo linamaanisha kuwa jeshi la Mahdi halitashambulia majeshi ya marekani na mengine ya shirika nchini Iraq.Hata hivyo wawakilishi hao hawakueleza iwapo watalipiza kisasi endapo jeshi la Mahdi linashambuliwa.

Wakati huohuo Waziri mkuu wa Iraq Nuri al Maliki ametangaza muda wa kutotembea mjini Karbala baada ya mapigano makali kutokea na kusababisha vifo vya watu 52.Maelfu ya Washia wanakutana mjini humo ili kuadhimisha sherehe ya kidini ya Kishia ya Shabaniya.

Bwana Maliki anawalaumu wafuasi wa kiongozi wa zamani wa Iraq marehemu Saddam Hussein kwa kuanzisha ghasia hizo.Majeshi ya usalama ya Iraq yanadhibiti mji kwa sasa.Muda huo wa kutotembea ulianza saa moja za London na unahusisha watu pamoja na magari kwa mujibu wa tangazo la televisheni ya kitaifa.

Mapigano hayo yalisababisha mahujaji hao kutoroka.Sherehe za Shabaniya ni za kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Imam Mohammed al Mahdi katika karne ya 9.Imam huyo wa 12 wa kishia alipotea mjini Samarra na kuepuka mauti ila atarejea kuuokoa ulimwengu.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com