1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Gates amaliza ziara yake Irak

22 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChA

Waziri wa ulinzi wa Marekani, Robert Gates, amekamilisha ziara yake rasmi nchini Irak hii leo. Ziara yake ililenga kutafuta mbinu mpya katika vita vya Irak ambavyo amesema Marekani haishindi wala haishindwi.

Wakati huo huo jeshi la Marekani limetangaza kuwa wanajeshi wake wanne wameuwawa walipokuwa wakishika doria katika mkoa wa Anbar, ngome ya upinzani wa wasunni dhidi ya majeshi ya Marekani na Irak.

Kuuwawa kwa wanajeshi hao kumeiongeza idadi ya vifo vya wanajeshi wa Marekani kufikia 2,959 na kuongeza shinikizo dhidi ya rais George W Bush wa Marekani atafute mkakati utakaowawezesha wanajeshi wote wa Marekani waondoke kutoka Irak.

Rais Bush amesema atatangaza mpango mpya mwezi Januari mwakani baada ya kusikiliza ushauri wa makamanda wa jeshi, maofisa wa wizara ya mambo ya ndani, viongozi wa Irak na waziri Gates.