Baghdad. Bomu laua watu 26 katika mtaa wa maduka ya vitabu. | Habari za Ulimwengu | DW | 05.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Baghdad. Bomu laua watu 26 katika mtaa wa maduka ya vitabu.

Bomu limelipuka katika mtaa wenye maduka mengi ya vitabu mjini Baghdad na kuuwa watu 26 na kusababisha kuungua moto kwa maduka kadha na magari hii leo.

Polisi wamesema kuwa mlipuko huo katika mtaa wa Mutanabi umeua watu 26 na kuwajeruhi wengine 54.

Watu walioshuhudia wamesema kuwa mlipuko huo umesababishwa na mtu aliyejitoa muhanga.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com