BAGHDAD: Al-Maliki akutana na viongozi wa Kisunni | Habari za Ulimwengu | DW | 18.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Al-Maliki akutana na viongozi wa Kisunni

Waziri Mkuu wa Irak,Nuri al-Maliki anakutana na viongozi wa madhehebu ya Kisunni katika mji wa Tikrit,ambao ni mji alikotokea kiongozi wa zamani Saddam Hussein.Azma ya mkutano huo ni kuwashawishi viongozi hao kuunda ushirikiano mpya ili kuiokoa serikali inayoporomoka.

Kiongozi huyo wa Kishia amesema,atazungumza na maafisa wa Kisunni wa eneo hilo walioungana nae kupigana dhidi ya makundi ya Al-Qaeda,ikiwa atashindwa kupata makubaliano pamoja na wanasiasa mashuhuri wa Kisunni.Ziara hiyo inafanywa siku moja baada ya Rais al-Maliki kutangaza muungano mpya kati ya Washia na Wakurd kwa matumaini ya kuiokoa serikali yake inayodhibitiwa na Washia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com